Kumekuwa na jaribio lililotibuka la kumuua kaimu
waziri wa ndani nchini Libya Al-Sidik Abdel-Karim.
Shirika la kitaifa la habari LANA na lile la AFP yamethibitisha tukio.
Inaarifiwa kwamba gari alimokuwa Abdel Karim lilipigwa risasi alipokuwa
akielekea katika mkutano katika makao makuu ya bunge.
Abdel-Karim anatarajiwa kuhutubia waandishi habari hivi punde.
Libya imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa kisiasa tangu Muamar Gadaffi kuuawa
Abdel Karim aliteuliwa na waziri mkuu nchini Libya kuwa kaimu waziri
wa ndani baada ya waziri Mohamed Sheikh kujiuzulu mnamo Agosti mwaka
jana.
Seddik Abdelkarim, alikuwa katika gari lake
aliposhambuliwa na watu wasiojulikana waliomfyatulia risasi. Inaarifiwa
hakuna aliyeuawa kwenye shambulizi hilo.
Libya imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya
kisiasa tangu waasi kuipindua serikali na kumuua aliyekuwa Rais Muamer
Kadhafi mwaka 2011.
Waziri huyo alikuwa njiani kuelekea bungeni wakati gari lake liliposhambuliwa.
Shambulizi lenyewe limetokea chini ya wiki tatu
baada ya mauaji ya naibu waziri wa viwanda Hassan al-Droui, aliyeuawa
mjini Sirte
0 Comments