Umoja wa mataifa umetuhumu makao makuu ya kanisa katoliki la
Vatican kwa
kuidhinisha na kutumia sera zilizowezesha mapadre
kubaka na kuwalawiti
maelfu ya watoto.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukifuatilia visa vya mapadre kuwadhulumu watoto
Kamati ya umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema kanisa hilo
linapaswa kuondoa wote wanaokiuka haki za watoto kutoka nafasi za
uongozi na kuanzisha uchunguzi dhidi yao.
Kamati hiyo imekiri kuwa japo Vatican imeshiriki mazungumzo na kuahidi mageuzi, bado inahitaji kupiga hatua kubwa zaidi.
Mengi yaliyoandikwa katika ripoti hii yamekuwa
yakiangaziwa na vyombo vya habari. Shutma hizo ni pamoja na kuharibu
watoto, kuwapa adhabu kali na kuwatenganisha na wazazi wao.
Umoja wa mataifa unasema uongozi wa kanisa katoliki unapaswa kufanya juhudi zaidi ili kuzuia makosa yaliyowahi kutokea.
Umoja wa mataifa pia umesifia marekebisho
yalioyafanywa katika sheria za Vatican lakini umesema kwamba utekelezaji
unahitajika kwa kasi.
Kwa upande wake kanisa katoliki limekiri kwamba
linahitaji kuhakikisha kwamba sheria zake zinaambatana na sheria za
umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
Ripoti hiyo pia imekosoa msimamo wa Kanisa katoliki mapenzi ya jinsia moja,upangaji uzazi na uavyaji mim
0 Comments