Watu wapatao 2000 wahofiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan, Afghanistan
Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.
0 Comments